
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameanza kazi rasmi katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Kombo ameanza majukumu hayo muda mfupi baada ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri January Makamba (Mb).
Makabidhiano hayo yalihudhuriwa pia na Naibu Mawaziri ambao waliteuliwa pamoja, Mhe. Cosato Chumi na Mhe. Dennis Londo

Waziri katika siku yake ya kwanza amekutana na kufanya mazungumzo na Mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndungulile.
Aidha, Mhe. Waziri amekutana na baadhi ya Wakurugenzi waliopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ambapo amepoeka taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
