×

Mwili wa Mama Mzazi wa Halima Mdee Waagwa Dar, Kuzikwa Kilimanjaro

MWILI wa Mama mzazi wa Mbunge wa viti Maalum, Halima James Mdee umeagwa leo katika kanisa katoliki la Ubungo Kibangu  jijini Dar es salaam na kusafirishwa kuelekea Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.

Kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na viongozi wengine wa kisiasa akiwemo Mwenyekiti wa Cahama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA0 Freeman Mbowe ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza katika kutoa heshma zao za mwisho.

Mamam mzazi wa Halima Mdee aitwaye, Theresia Mdee alifariki dunia asubuhi ya Jumanne Julai 30, 2024, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma baada ya kuugua saratani ya shingo ya kizazi. Mwili wa marehemu ulisafirishwa kutokea Dodoma kisha jijini Dar es Salaam ambapo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 umepelekwa Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi.

Baba Mzazi wa Halima Mdee akiwa mwenye majonzi mazito Kanisani.
Mwili wa Mama Mzazi Halima Mdee aitwaye Theresia Mdee ukiingizwa kanisani kwa ajili ya sala ya kumuombea.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (kulia) akiwa kanisani wakati ibada ya kumuombea sala ya mwisho mama mzazi wa Halima Mdee ikiendelea.
Sehemu ya wanafamilia walipokuwa wameketi wakati ibada ikiendelea.

Leave a Comment