×

“Ndoa za mama zetu zilitetereka, make-up hazikukaa usoni ksababu ya maji” – Aweso

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Ifakara wilayani Ifakara mkoani Morogoro leo Jumatatu tarehe 05 Agosti 2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

“Tulishuhudia make-up za wanawake hazikai kisa hakuna maji Mheshimiwa Rais, ndoa za mama zetu zilitetereka, tulishuhudia ziara za viongozi zilipokelewa na madumu ya maji, lakini Mheshimiwa Rais ulivyoingia ukaasisi kaulimbiu yako ya kwenda kumtua mama ndoo kichwani” – Aweso.

Aidha, Akizumgumza na wananchi wa Ifakara Waziri Aweso amesema mji wa Ifakara unanufaika na Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoitwa Kiburubutu wenye thamani ya Bilion 42 na mkandarasi yupo eneo la kazi pia Mradi umefikia Asilimia 23% na utazalisha lita milion 20 kwa siku.

Pia amesema kwamba Mahitaji ya Maji kwasasa ni lita Mil.9.6 na Uzalishaji ni Lita Mil.3 kukiwa na Upungufu Lita Mil. 6
Kukamilika kwa mradi wa Kiburubutu utaweza upatikanaji Maji kwa asilimia 100% mjini Ifakara.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Ifakara wilayani Ifakara mkoani Morogoro siku ya Jumatatu Agosti 5, 2024 wakati wa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani humo.

 

Leave a Comment