×

Chatanda afurahishwa na utekeleza wa miradi Tisa ya maendeleo Jimbo ya Buchosa na Sengerema

Mwenyekiti wa Uwt Taifa Mary Chatanda amepongeza wabunge wa Sengerema na Buchosa Eric Shigongo Hamis Tabsamu kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye majimbo yao.

Kauli hiyo ameitao alipokuwa akikagua ujenzi wa kituo cha afya Nyakasungwa kilichopo Jimbo la Buchosa huku akisema wabunge hao wanafanya kazi nzuri za kusimamia miradi na hiyo ambayo inatolewa fedha na Rais Samia Suluhu Hassan.

Miradi hiyo inathamani ya Sh 1.4 bilioni ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa kituo cha afya Nyakasungwa, Shule ya msingi Kijiweni na shule ya msingi mlimani iliyoko Kata ya Kahunda.

Amesema wabunge hawa wanapaswa kupewa sifa ya kazi wanazozifanya za kuwahudumia wananchi wako katika nyanja ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Sambamba hilo amepongeza mkurugenzi wa Buchosa Benson Mihayo Kwa kutenga kiasi cha Shilingi milioni 150 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa kituo ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi milioni 83 zimekwisha tumika na kujenzi unaendelea na ndani ya muda mfupi kituo hicho kitakuwa kimekamilika.

Leave a Comment