
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na vyuo vinavyotoa mafunzo ya kilimo kwa kuongeza tija mashambani, hayo yamesemwa leo Agosti 6, 2024 kwenye ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro.
Aidha Rais Samia ameipongeza miradi mbalimbali inayozalishwa na Chuo hiko ikiwa pamoja na kutoa mafunzo kwa vikundi na kuwapatia ajira, pia amevitaka Vyuo vingine viige kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine.



