×

Mzee Magoma Ashindwa Kesi, Kuilipa Yanga Mil 60

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali mwenendo nzima wa maombi yaliyofunguliwa na Juma Magoma na wenzake ya kutaka kuundoa uongozi wa Klabu ya Yanga madalakani na pia kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi wazee hao.
Aidha, Mahakama hiyo imemuaru Magoma, Geofrey Mwaipopo na Abeid Mohamed Abeid walipe muombaji ( Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga) gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
Uamuzi huo, umetolewa leo Agosti 9, 2024 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga wa mahakama hiyo, wakati akitoa uamuzi wa
marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022 yaliombwa na bodi hiyo kwa madai kuwa wazee hao hawakuwa na sifa ya kufungua shauri.
Hakimu Kiswaga amesema bodi hiyo iliwasilisha maombi manne ya kuomba kufanya marejeo, ambapo mahakama imekubali matatu na moja imelitupilia mbali kwa madai kuwa halina mashiko kisheria.
Amesema kuwa sababu ya kwanza ni kwamba, bodi hiyo inadai kuwa Magoma na wenzake walipeleka maombi yao kwenye mahakama ambayo haina mamlaka ya kuyasikiza ambayo ni Mahakama ya Kisutu.
Alisema sababu ya pili, Mahakama inaona haina mashiko kwa sababu ili mahakama iweze kufanya marejeo hapaswi kwenda kuangalia ushahidi, suala la kwamba walitakiwa kutoa kadi za uanachama ili kuhalalisha uanachama wao ni suala la ushahidi.
Pia, alisema sababu ya tatu, Magoma na Mwaipopo walitakiwa kufungua shauri la kwa hati ya madai na sio maombi kama walivyowasilisha wao, jambo ambalo mahakama imeona ni sababu ya kuikubalia bodi hiyo kufanya marejeo ya shauri hilo.
Hakimu huyo, amesema kwa sababu hizo mahakama inaona maombi ya marejeo yana mashiko, kwa hiyo imekubali Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga kufanya hivyo.
Ilidaiwa kuwa Novemba 6, mwaka 2022, watu wawili waljiita wanachama wa Yanga walifungua shauri, ambai ni Juma Ally (Magoma) aliyekuwa mlalamikaji namba moja na Geofrey Mwaipopo ambaye ni mlalamikaji namba mbili na wa tatu ni Jabir Katundu ambapo walifungua dhidi ya Baraza la Wadhamini kama mlalamikiwa namba moja, Fatma Karume, Abeid Mohamed Abeid, ambaye ni mlalamikiwa namba ikidaiwa walichokuwa wakihitaji ni kuondoka kwa viongozi waliopo, na mali za klabu na timu wakabidhiwe wao.
Mkurugenzi wa sheria wa Klabu  ya Yanga, Saimon Patrick (kushoto) na mawakili wenzake, wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam baada ya kushinda maombi ya marejeo dhidi ya Juma Magoma na wenzake, ambapo wanatakiwa  kulipa gharama za Kesi.

Leave a Comment