×

BRITAM, Bank of Africa Zashirikiana Kuongeza Upatikanaji wa Huduma za Bima ya Afya

Britam Insurance Tanzania na Bank of Africa zashirikiana kuongeza upatikanaji wa huduma za Bima za Afya Tanzania ziitwazo ‘Amani Health’ na ‘Afya Care’

Ushirikiano huo unalenga kuongeza wigo mpana kwa wateja wa ‘Bank of Africa’ ili kuhakikisha kuwa watu binafsi, familia, wafanyabiashara na vikundi rasmi wanapata huduma za afya zenye unafuu na viwango. ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’ zitakidhi mahitaji mbalimbali ya matibabu ya wateja wa Bank of Africa, katika kupunguza gharama za kifedha wakati wa dharura zinazohusiana na afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania, Farai Dogo alieleza kufurahishwa kwake na ushirikiano huo na kusema, “Tunafuraha kuungana na Bank of Africa nchini Tanzania ambapo tumeweza kuwaletea wateja wao huduma hizi muhimu za ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’.

“Ushirikiano huu unaendana na dhamira yetu ya kuhakikisha tunatoa huduma bora za afya kwa watanzania wote. Hivyo ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi na kuwapa ulinzi wanaohitaji ili waishi maisha bora zaidi.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi. Esther Cecil Maruma, alisema “Ushirikiano wetu na Britam Insurance Tanzania ni uthibitisho wa ari yetu ya kutoa huduma za kipekee kwa wateja wetu, kupitia ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’.

“Hii sio tu kwamba tunaboresha utoaji wa bidhaa zetu lakini pia tunahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma muhimu za afya. Mkakati huu unaonesha dhamira yetu ya kuboresha ustawi kwa wateja wetu na jamii inayotuzunguka.”

“Bidhaa hizi zitapatikana kwa wateja wetu kuashiria hatua kubwa ya kuongeza upatikanaji wa huduma za afya na kuongeza wigo wa bima nchini Tanzania” akisistiza Bi. Eva Daudi Kakwale, Afisa Mkuu wa Idara ya Bima wa Bank of Africa Tanzania.

George Mwita, Meneja wa Idara ya Afya, Britam Insurance Tanzania, alisema “Tunaamini kwamba ushirikiano huu utaongeza kiwango kipya cha bima ya afya nchini Tanzania.

“Uzinduzi wa bima hizi ni sehemu ya mkakati unaoendelea katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya na huduma ya bima nchini Tanzania huku tukiunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bima ya afya inapatikana kwa watu wote.

“Britam Insurance Tanzania na Bank of Africa Tanzania zimejitolea kuhakikisha kuwa bidhaa hizi zinaleta matokeo chanya katika maisha ya wateja wao.

Kwa habari zaidi tafadhali tembelea matawi ya Bank of Africa na Britam Insurance Tanzania lililo karibu nawe.

Leave a Comment