×

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Sumbawanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kuzingatia kibali cha ajira chenye Kumb.Na. FA.97/228/01/09 cha tarehe 25/06/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, anakaribisha maombi ya kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 19 za kazi kama ifuatavyo:

BONYEZA HAPA >>>Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Sumbawanga

 

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya
Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa
kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye
anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika;
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na  Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya
Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
vii. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato
cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 22 Agosti, 2024.
xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja
na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –

Leave a Comment