
Mfanyakazi wa ndani, Clemensia Milembe (19) na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni, wakikabiliwa na shitaka moja la kujaribu kuua.
Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ni Elizabeth Makori (38) maarufu kama mama Brayan, mkazi wa Goba kinzudi.
Washtakiwa hao wakabailiwa na kesi ya kujaribu kuua kinyume na kifungu 211 kifungu kidogo (a) cha Sheria ya Adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Washtakiwa wote ambao ni wakazi wa Goba, wamefikishwa mahakamani hapo leo Agosti 15, 2024 na kusomewa shitaka hilo na wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalila.
Katika kesi hiyo, Wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu amedai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wanakabiliwa kesi ya kujaribu kuua namba 22964/2024.
Akiwasomea shitaka lao, wakili Kamungu amedai washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 15, 2024 katika eneo la Goba Kizundi iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni.
Inadaiwa siku ya tukio, washtakiwa kwa pamoja walijaribu kusababisha kifo kwa mtoto Maliki mwenye umri wa
Miaka sita.
Baada ya kusomewa shtaka hilo hakimu amedai mahaka hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo hadi mahama kuu.
Hakimu Rugemalila amedai kuwa dhamana ya washtakiwa hao ipo wazi hivyo kila mmoja anatakiwa kusaini bondi ya mil 10 na wadhamini wawili ambao kama ni mfanyakazi wa serikali atawasilisha barua kutoka kwa mwajiri wake ama kuwa na baru mbili kutoka serikali ya mtaa inayomtambulisha mdhamini husika.
Mshtakiwa wa kwanza Clemensia hakuwa na mdhamini hata mmoja huku mshtakiwa wa pili akiwa nao licha ya mmoja kushindwa kutimiza masharti na kesi imeahirishwa hadi Agosti 29,2024.