×

Rais Dkt. Samia Atoa Vyeti Vya Mafunzo Uwanja Wa Mwehe Makunduchi Zanzibar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi vyeti Wahitimu wa mafunzo ya Kilimo Biashara, Ujasiriamali pamoja na Utalii kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 20 Agosti, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akitoa Vyeti vya Mafunzo Uwanja wa Mwehe Makunduchi Zanzibar, leo tarehe 20 Agosti, 2024.

Rais Samia amesema shughuli za uvuvi katika Pwani hususan upande wa Zanzibar, zimesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ambao unaonekana vizuri ukisafiri kwa anga.

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa hafla ya kutoa vyeti vya mafunzo, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi jijini Dar es Salaam.

Matukio Mbalimbali wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Skuli ya Maandalizi Dkt. Samia Suluhu Hassan katika shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi.
Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi, Makunduchi, Shehia ya Tasani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa maeneo ya jirani na Tasani mara baada ya hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.
Rais Sami akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 63.8 kutoka Asasi ya Sekta Binafsi inayojishughulisha na kuendeleza sekta ya Horticultural Tanzania (TAHA) kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kilimo biashara.
Rais Samia  akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Rais Samia Suluhu akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 30 kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Leave a Comment