
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Ramadhani Nga’zi amesema hadi kufikia Agosti 26 mwaka huu vyombo vyote vya moto vinatakiwa viwe vimefanyiwa ukaguzi na kwa wamiliki watakao kouka agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
DCP Nga’zi amesema hayo wakati akizunguzma na waandishi wa habari Katika halfa ya uzinduzi wa miaka 50 ya baraza na wiki ya nenda salama kwa mwaka 2024 iliyobeba kauli mbiu isemayo endesha salama fika Salama inayoenda sambamba na utoaji elimu kwa wamiliki na watumiaji wa vyombo vya usafiri.
Amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpango mkakati ambapo baraza la Usalama barabarani litazindua mpango mkakati wa kupambana na ajali za barabarani.
Amesema kuwa kila Dereva anatakiwa kuwa makini anapokuwa barabarani kwa kuzingatia usalama wa Chombo chake ,watembea kwa miguu na watu wote wanaotumia barabara ili kuondoa ajali zisizo za lazima.
Kwa upande wake Naibu kamishna wa polisi Mstaafu na mjumbe wa Baraza la Usalama Barabarani Mohamed Mpinga amesema Jambo la Usalama barabarani ni la kila mtanzania hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya usalama siku ya maadhimisho hayo.
Wiki ya usalama barabarani nchini itaadhimishwa agost 26 ambapo makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzanaia Dk Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.