×

Makamu Wa Rais Alivyokabidhi Ubingwa Kwa Mshindi Wa Kizimkazi Samia Cup 2024- Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akikabidhi Kombe kwa Mabingwa wa Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 ambayo ni timu ya Shule ya Sekondari Kusini mara baada ya kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0 katika mchezo wa fainali uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar tarehe 24 Agosti 2024 ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akifuatilia mchezo wa mpira wa miguu fainali ya Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 baina ya Shule ya Sekondari ya Kusini na Shule ya Sekondari Muyuni.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amekabidhi Kombe kwa Mabingwa wa Kizimkazi Samia Youth Cup 2024 kwa timu ya Shule ya Sekondari Kusini mara baada ya kuifunga Shule ya Sekondari Muyuni jumla ya magoli 3-0 katika mchezo wa fainali uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar  Agosti 24, 2024 ikiwa ni shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi.

Leave a Comment