×

CCM Ni Imara Wakati Wote, Tutarajie Ushindi wa Heshma- CPA Makalla

 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makala amewataka wanachama wa hicho pamoja na wananchi kuwachagua wagombea watakaotokana na Chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

CPA Makala ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam amesema zipo sababu za msingi za CCM kushinda ushindi wa heshima katika uchaguzi huo wa Serikali Mitaa mwaka huu kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana yakiwemo ya utekelezaji wa Ilani katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Akizungumza wilayani Kigamboni alipokuwa akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara CPA Makala amesema kwamba mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambako ndiko ndio maamuzi ya wananchi wanafanya katika kuchagua viongozi wao ,hivyo ni uchaguzi muhimu.

“Mimi pamoja na Viongozi wenzangu akiwemo Katibu Mkuu wetu Balozi Nchimbi tumefanya Mikutano Mikoa mbalimbali tumejionea mambo makubwa kila Kona  CCM imekuwa imara sana kwenye kipindi hiki kwani kila sehemu tunapokanyaga ni pongezi kwa Chama cha Mapinduzi kwani Utekelezaji bora wa Ilani umefanyika hii imetupa ishara tosha ya kukubalika na hata Ile Mikoa tuliyobakisha niwaambie tutafika Mikoa yote” .

“Lakini kuna sababu zinazofanya CCM iwe imara na kushinda Uchaguzi ujao kwa kishindo ni kwa sababu ya Utekelezaji bora wa Ilani ya CCM kwani kwa asilimia kubwa kila sehemu kuna maendeleo na Wananchi wamekubali lakini tutashinda Uchaguzi sababu ya wenzetu wanaojiita Vyama vya Upinzani nako kuna fuka Moshi watu wamegawanyika hivyo sisi tunaendelea kufurahia la Mwisho tutashinda Uchaguzi kulingana na kuongeza kwa Wanachama wa chama cha Mapinduzi kila uchwao watu wanahamia na wapya wanazidi kujisajili kwakweli tutashinda kwa kishindo”.
Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo Ndugu CPA Amos Makalla amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Kigamboni katika Viwanja vya Tungi Mnadani.

Leave a Comment