×

LHRC Yazindua ripoti ya 10 haki za binadamu na biashara tanzania 2023/24


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeendelea kufanya utetezi wa haki za binadamu katika sekta ya biashara ambapo kimekuwa kikifanya uchechemuzi wa sera na kuhakikisha mikataba na miongo ya kimataifa pamoja na Sheria za nchi zinahusiana na biashara zinatekelezwa kwa kuzingatia haki za binadamu.

Kituo hicho kimekuwa kikitoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa shughuli za biashara kufanya tafiti na kuchapisha taarifa ya hali ya haki za binadamu katika sekta ya biashara ili kubainisha wajibu wa serikali kulinda haki za binadamu katika sekta ya biashara, wajibu wa makampuni kuheshimu haki za binadamu na kutoa nafuu ya kisheria kwa wahanga wa haki za binadamu.

Tangu mwaka 2012, Kituo hicho kimekuwa kikitoa taarifa ya haki za binadamu na biashara, kwa muktadha huo, Kituo hicho kimeandaa na kukamilisha taarifa ya haki za binadamu na biashara ya mwaka 2023/2024 ambayo imezinduliwa leo August 27.

 

Taarifa hiyo sio tu imebainisha matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu bali pia imetoa mapendekezo kwa ajili ya uboreshaji wa sera, sheria na utendaji katika jamii na kubainisha baadhi ya mambo muhimu yaliyojitokeza katika taarifa hiyo iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dkt. Anna Henga imebaini asilimia 69.4% ya wafanyakazi wanaendelea kuripoti kufanya kazi bila kupewa mikataba ya ajira kutoka kwa waajiri, ikilinganishwa na mwaka 2021/2022 kuna ongezeko la takribani asilimia 4.8% katika eneo hilo, ambapo mwaka 2021/2022 asilimia 64.6% ya wafanyakazi walilalamika kukosa mikataba ya ajira.

Haki za makundi maalumu, wanawake na watu wenye ulemavu wameendelea kuwa wahanga wakubwa katika upatikanaji wa ajira, huduma na mazingira muhimu kulingana na uhitaji wa makundi hayo.

Uelewa kuhusu uwepo wa vyama vya wafanyakazi, asilimia 37% pekee ndio wanatambua uwepo wa vyama vya wafanyakazi nchini, ambapo changamoto hiyo inaendana na changamoto nyingine kama kufukuzwa kazi kinyume na utaratibu na Sheria za nchi, kutonufaika na mifuko ya hifadhi za jamii, pamoja na kiwango cha mshahara kisichoendana na gharama za sasa za maisha.

Haki ya kumiliki ardhi, changamoto zilizoelekzwa katika eneo hilo ni ucheleweshwaji wa malipo ya fidia, tathimini ya ardhi isiyoendana na hali ya maisha pamoja na ushiriki shwajwi mdogo wa wananchi katika utwaaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli za uwekezaji, hususan katika maeneo yenye shughuli za uwekezaji.

Haki ya mazingira, changamoto za kimazingira zimeendelea kuonekana, hasa kwenye uchafuzi wa hewa na ardhi ambapo makampuni mengi hayana sera za mazingira zenye ufanisi wa kutunza na kurudi sha hali ya mazingira baada ya shughuli za uwekezaji ambapo ni takribani asilimia 46% pekee ya makampuni yameonekana kuwa na sera za utunzaji wa mazingira.

Uwajibikaji wa makampuni mengi yameonekana kurudisha kwa jamii zaidi kwenye sekta ya elimu na afya, takribani asilimia 56% ya wanajamii wamekubali kunufaika na makampuni yanayorudisha kwa jamii ambapo makampuni hayo yameonekana kukiuka zaidi haki za kazi, ajira na haki za mazingira katika utendaji wa shughuli za biashara.

Ripoti hiyo imesomwa mbele ya mgeni rasmi Mh.Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu pamoja na wageni kutoka sehemu mbalimbali walioudhulia uzinduzi huo.

Leave a Comment