×

Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Kampeni ya Raila Odinga AU (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Dkt. William Samoei Ruto, Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti 27, 2024 akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Dkt. William Samoei Ruto, amesema Tanzania inamuunga mkono Raila.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mhe. Dkt. William Samoei Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya pamoja na Viongozi wengine wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Ikulu ya Nairobi, tarehe 27 Agosti, 2024.
Rais Samia akiwa kwenye picha na Dkt. William Samoei Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya.
Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya akizindua kampeni ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Ikulu ya Nairobi.

>

Leave a Comment