×

Rais Samia Alivyowasili Arusha Kufungua Mkutano Wa CEO’s Forum 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro tayari kwa kuelekea mkoani Arusha ambapo ni Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) tarehe 28 Agosti, 2024. Dkt. Samia amewasili uwanjani hapo akitokea nchini Kenya ambapo alihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), tarehe 27 Agosti, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Arusha  Agosti 27, 2024 kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu Rais Samia amepangiwa kufungua Kikaokazi cha Wenyeviti wa bodi na Watendaji wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za serikali (CEO’s FORUM 2024) Mkutano unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC Jijini Arusha.

Kikaokazi hicho kinachozinduliwa Jumatano hii Agosti 28, 2023, kina lengo la kuwafahamisha na kuwashirikisha maafisa hao juu ya maboresho yanayoendelea katika kuimarisha usimamizi, uendeshaji na utendaji wa Taasisi za umma sambamba na kubadilishana uzoefu kwa watendaji hao.

  

Leave a Comment