
Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM Kichama Mkoa wa Dar es salam Agosti 29, 2024 amehitimisha ziara yake ya kukagua na kusikiliza kero za wananchi katika majimbo 10 ya Mkoa wa Dar es salam akimalizia Jimbo la Mbagala .
Mwenezi Makalla akihutubia Maelfu ya Wanachama na Wananchi wa Wilaya ya Temeke Jimbo la Mbagala viwanja vya Maturubai amesema kwa Wingi huu mmenitia moyo kuwa CCM bado ni imara sana na itaendelea kuongoza Nchi hii nami niwapongeze kwa mapokezi Makubwa na Mazuri na huu Ujumbe ni nitamfikishia Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mbagala wamezima zote na wamewasha Kijani.

