Sharif Abdallah Ali, mdogo wa marehemu Ali Kibao, ameeleza kuhusu uamuzi wa familia kutokana na kifo cha ndugu yao.
Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho ambapo siku chache zilizopita, ilidaiwa kwamba ametekwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya basi, akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga.
Muda mfupi baadaye, ndipo zilipopatikana taarifa kwamba mwili wake umeokotwa katika Viwanja va NSSF, Ununio jijini Dar es Salaam na baadaye kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala.