×

Rais Samia ataka uchunguzi wa kina kufuatia kifo cha afisa wa Chadema

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii- Rais Samia Suluhu Hassan.

RAIS SAMIA ATAKA TAARIFA za WALIOMUUA MZEE ALI KIBAO HARAKA – ”TUKIO HILI BAYA KABISA”

Leave a Comment