×

Boniface Jacob Apandishwa Kisutu, Asomewa Mashtaka Mawili ya Kusambaza Taarifa za Uongo

Meya mstaafu wa manispa a kinondoni Bonifqce Jacob amefikishwa mahakamani leo na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga huku akitetewa na Jopo la Mawakili akiwemo Peter Kibatala na Hekima Mwasipu.

Katika kosa la kwanza linalomkabili Boniface Jacob linahusu kuchapisha taarifa za uongo mnamo tarehe 12 Septemba 2024, ambapo alidai kuwa Mafwele anatuhumiwa na familia nyingi kwa kupotea kwa wanafamilia wa hizo familia.

Katika Kosa la pili, inadaiwa lilitokea tarehe
14 Septemba 2024, na linahusiana na kuchapisha taarifa nyingine za uongo zinazosomeka ‘Polisi wanatesa watu na kuua ndio kazi wanaweza.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Boniface amekana mashtaka yote hayo ambapo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Nasoro Katuga umewasilisha maombi tena mawili ambayo ni kupinga Meya wa zamani wa Ubungo kupewa dhamana katika mashtaka mawili yanayomkabili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo ambayo hadi sasa usikuu wa saa 2 mvutano wa mawakili unaendelea.

Katika maombi hao ni kwamba wanaiomba mahakama itoe amri kwa mjibu maombi kuruhusu kupekuliwa akaunti yake ya X na kutoa Password ili kurahisisha uchunguzi wa akaunti hiyo inayoendana na makosa yake.

Pia ombi la pili, upande wa Jamhuri umeleta ombi la kuahirisha kama si kupinga mshtakiwa kupewa dhamana kwa sababu za usalama wa mshtakiwa huyo.

Leave a Comment