
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimempongeza Rais DK Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake aliyoitoa Kilimanjaro ya kukemea vitendo vya utekaji na mauaji huku akiliagiza jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini wale wanao husika na vitendo hivyo huku kikilaani vitendo hivyo vya upotoshaji wa hotuba hiyo vinavyofanywa na wapinzani hususan Chadema.
Pia, alisema CCM imejipanga vizuri kushinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dk.Samia ya kutekeleza miradi mikubwa na kupeleka fedha nyingi vijijini za utekelezaji miradi ya maendeleo.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya siasa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mheshimiwa Rais alitoa kauli ile, akiwa Rais, kiongozi mkuu wa nchi na Amiri jeshi Mkuu, alitoa kauli Ile lakn watu wenye Nia mbaya wamekuwa mitandao na wengine katika vikao vyao wamekuwa wakipotosha na kulipa maana nyingine,
“Nataka niseme mheshimiwa Rais Baada ya taarifa za kifo Cha Kibao, alitoa pole na kutoa maagizo ya kufanyika uchunguzi Kwa kina, alitoa pole Kwa masikitiko makubwa tofauti na wengine wanavyo potosha kauli na maagizo ya Rais Dk.Samia,” alisema.
Aliongeza “CCm kupitia Mwenezi nilitoa pole na siku hiyo Rais alitoa pole na maelekezo ya uchunguzi wa kina, kwa kusikitishwa na kifo hicho, vivyo kwa Rais na Watanzania wote Kila mmoja hili jambo lilimshtua, na alitaka lisijirudjie tena, inapotokeq jambo la kifo, wote linatusikitishaa,” alisema.
Alisema chaajabu baada ya hotuba Ile kimekuwepo upotoshaji na kauli zingine ambazo hazina maana kwa hiki tuweke wazi Rais Samia ametaka lichunguzwe.
Alisema upinzani kupitia Mwenyekiti wao wamekuwa wakitoka kauli tofauti za kutokubaliana na uchunguzi,
Pia alisema kuna mikakati ya Chadema ya kuchafua nchi yetu, hawapendezwi na amani na maendeleo makubwa yaliyopo
Alisema linalo wap shida Chadema ni utendaji mkubwa wa Rais Dk.Samia na kupeleka fedha nyingi vijijini kuliko awamu nyingine, miradi mikubwa imeendelea kutekelezwa, ikiwemo Bwawa la Mwalimu lililojengwa, Reli ya Kisasa, mradi wa kununua ndege ambazo wanazitumia.