
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
-MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II – (NAFASI 2)
-DEREVA DARAJA LA II NAFASI (2)
-DEREVA WA MITAMBO DARAJA LA II NAFASI (1)
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28/09/2024.