×

Jeshi la Polisi Lamjibu Rais wa TLS, Wakili Mwabukusi Kuzuia maandamano ya vyama vya siasa

Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi David Misime.

Jeshi la Polisi nchini kupitia msemaji wake David Misime, limetolea ufafanuzi wa maoni ya baadhi ya watu na makundi mbalimbali ya watu, akiwemo rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika Boniphase Mwabukusi kuwa, Jeshi hilo halina mamlaka ya kuyazuia maandamano ya vyama vya siasa isipukuwa wana wajibu wa kuyasimamia na kuyasindikiza kuhakikisha kuwa yanafanyika kikamilifu.

Leave a Comment