
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Bandari ya Mbambabay mkoani Ruvuma 25 Septemba 2024.
Ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbamba Bay iliyopo katika wilaya ya Nyasa umeelezwa kugharimu zaidi ya Shilingi bilioni 80 mpaka kukamilika kwake huku ukitegemewa kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika Ushoroba wa Kusini.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassani Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema mradi huo utakapokamilika utafungua fursa za kibiashara kati ya nchi ya Tanzania na nchi za Zambia,Malawi na Msumbiji na kuhamasisha uwekezaji zaidi katika sekta binafsi na umma, hususan katika viwanda, usafirishaji, biashara, na utalii wa Ziwa Nyasa.
Naibu Waziri Kihenzile amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo kutapunguza msongamano katika bandari ya Dar es salaam na kuongeza ufanisi katika bandari ya mtwara na kuimarisha ushoroba wa kusini.
