
Waendesha baskeli zaidi ya 10 kesho asubuhi wakiwa wanatarajia kuanza safari ya kuelekea Butiama katika kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere leo wamemtembelea na kumuaga mjane wake, Mama Maria Nyerere.

Safari hiyo iliyodhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kesho asubuhi kwenye viwanja vya Posta jijini Dar huku waendesha baiskeli kutoka mataifa kadhaa ikiwemo Kenya, Kongo DRC na Burundi na nao wanashiriki mbio hizo.

Akizungumza nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, Dar kiongozi wa msafara huo, Gabriel Landa amesema wanatarajia kuanza msafara huo kesho majira ya alfajili ambapo wanatarajia kuwasili Butiama Oktoba 13 na kuungana na Watanzania wengine katika kumbikizi ya miaka 25 tangu kifo cha Hayati Baba wa Taifa. HABARI/PICHA RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL