×

TCRA Yasitisha Leseni ya Kampuni ya Mwananchi

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (kulia).

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha kwa muda wa siku 30 leseni za huduma za maudhui mtandaoni za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (The Citizen, Mwananchi Digital, Mwananchi na MwanaSpoti) kutoa huduma za maudhui mtandaoni nchini.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 2, 2024 na Mkurugenzi mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri K. Bakari imesema kampuni hiyo ilichapisha maudhui yaliyokiuka kanuni ambayo yameleta tafsiri hasi kwa Taifa, jambo ambalo linaathiri na kuharibu umoja, amani na mshikamano wa kitaifa

“Tarehe 01 Oktoba 2024 Mwananchi Communications Limited ilichapisha maudhui mjongeo na sauti (audio-visual content) kwenye mitandao yake ya kijamii, maudhui yaliyozuiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16 ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilizorejewa hapo juu.” imesema taarifa hiyo.

Leave a Comment