
Ziara ya Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi imeingia Siku yake ya Pili mkoani Simiyu, ambapo akizungumza na Wananchi katika Jimbo la Kisesa Wilayani Meatu, Baada ya Kuwasili ameahidi CCM itaendelea Kutatua Changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo Suala la Uvamizi wa Tembo kwenye Makazi na Mashamba pamoja na kuhakikisha Wafugaji ambao wameshinda Kesi Wanarejeshewa Mifugo yao.
Akizungumza na Wananchi katika Kata ya Mwandoya Wilayani humo, Pia Dkt Nchimbi ametolea Ufafanuzi mfumo wa Stakabadhi Ghalani, Changamoto ambayo imewasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina.

“Habari ya Stakabadhi ni Sera ya CCM, hiyo ni Bada ya Utafiti wa Kina ambao Ulifanywa na Wataalamu, kwa hii huu mfumo ni Sera rasmi inayoeleweka kwa Sababu Wananchi ndio walioridhia kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)” amesema Dkt Nchimbi.
Katibu Mkuu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC – Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Hamid Abdalla,
