
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja na kumbukumbu miaka 30 tangu kuanza kutoa huduma Tanzania, Kampuni ya simu ya Tigo imesafiri na baadhi ya wateja wake waliodumu kwa miaka yote kwenye kampuni hiyo kuelekea Dodoma na usafiri wa reli ya SGR.
Akizungumza mara baada ya kufika Dodoma, Afisa Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo, Isaack Nchunda, alisema Dhamira yao ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao muda wote.
“Kampuni ya Tigo ndiyo mtandao mkubwa wenye kasi zaidi Tanzania toka mwaka 1994 mpaka sasa ambapo ni historia ambayo imechangia maendeleo ya wateja wake binafsi na kufikia mafanikio mbalimbali,” amesema Nchunda.

“Tumekuja Dodoma na wateja wetu waliodumu na sisi kwa miaka yote kwenye kampuni yetu ili kuwahakikishia wateja wetu kwamba huduma zetu ni bora zaidi.”
Nchunda aliwasihi wateja wote kuendelea kutumia vifurushi vyao vyote ambavyo vimeboreshwa na vitaendelea kuboreshwa zaidi.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Tigo Pesa, James Sumari alisisitiza kwamba wataendelea kuboresha huduma zao ili wateja wote waendelee kupata huduma iliyo bora zaidi.
Afisa Biashara msaidizi wa Shirika la Reli Tanzania- TRC Dodoma, Betty Blasio alisema kwa Dodoma wana safari tatu asubuhi , safari ya saa 11:15 asubuhi, saa 8:10 asubuhi pamoja na 11:15 jioni hivyo aliwakaribisha wateja wote kufanya safari na TRC.

Husna Manyeki, Mteja wa Tigo Pesa Mkoa wa Iringa alisema yeye ni mteja wa Tigo Pesa tangu miaka ya nyuma hivyo alishukuru Tigo kwa kuendelea kutoa huduma bora na kuwasihi watu wote kutumia huduma za Tigo Pesa kwani ni rahisi na ni bora zaidi.
Huduma kwa wateja mwaka huu imeenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘Above & Beyond ‘ ambayo inathibitisha kwamba Tigo wako sako kwa bako na wateja wake. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL