Naibu Waziri Mkuu Ampongeza Makonda kwa Ubunifu wa kuitangaza Arusha
Global Publishers October 9, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Mashaka Biteko Naibu Waziri wa afya Dkt. Godwin Mollel na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda wakiwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha mikutano Jijini Arusha AICC leo Oktoba 09, 2024 kwaajili ya kufungua Mkutano wa mwaka wa wataalamu wa Mionzi barani Afrika, Mkutano unaofanyika kwa siku tatu mkoani Arusha.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Oktoba 09, 2024 amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda kwa ubunifu wake katika Uongozi, suala ambalo limechangia kuitangaza Arusha kimataifa na kuvutia wageni na mikutano mingi zaidi kwenye Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Mionzi kutoka barani Afrika kwenye Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Jijini Arusha, Naibu Waziri Mkuu amesifu pia mapokezi mazuri wanayoyapata wageni na Viongozi mbalimbali wanapokuja Arusha kwaajili ya shughuli mbalimbali na kusema ugeni huo umesaidia pakubwa kusisimua uchumi wa Mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Mashaka Biteko, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha – AICC, tayari kwa kufungua Mkutano wa mwaka wa wataalamu wa Mionzi barani Afrika, mapema leo Oktoba 09, 2024.
“PUUZENI UZUSHI DHIDI ya VIWANDA vya SUKARI – ILIKUWA DHARURA” – MARIAM DITOPILE…..