
Kipindi hiki ligi zimesimama kupisha michuano ya kimataifa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza umekaa kimtego mpaka sasa, Ambapo watu watatu wa nafasi za juu wakiwa wamekabana koo kwelikweli.
Liverpool wao wanaongoza msimamo wakiwa na alama 18 baada ya kucheza michezo 7 wakifuatiwa na Arsenal pamoja na Manchester City wote wakiwa na alama 17, Hii inakuonesha ni kwa namna gani timu hizo zimekabana koo kwenye msimamo.
Manchester City mpaka sasa haionekani kua kwenye ubora wake ambao imekua nao licha ya kukusanya alama 17 mpaka sasa, Lakini haionekana kucheza kwenye ubora wake wa kila siku ambao wamekua wakifahamika nao.
Majeraha ambayo yamekua yakiiandama klabu ya Manchester City msimu huu ni moja ya sababu ambazo zinawafanya wanashindwa kuonekana kwenye ubora wao, Rodri, Kevin de Bruyne ni miongoni mwa wachezaji muhimu ambao wamepata majeraha ndani ya klabu hiyo.
Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.
Manchester City mpaka sasa ni kama wanakuja wanakataa kutokana na naman klabu hiyo inavyocheza kutokana na kukosekana kwa wachezaji wake muhimu ndani ya kikosi, Lakini inaelezwa Pep Guardiola ana mpango wa kuingia sokoni katika dirisha kubwa lijalo ili kuirusisha timu hiyo kwenye ubora.