×

Gachagua: Nimenusurika Kuuawa Mara Mbili kwa Sumu – Video

Aliyekuwa Naibu Rais Nchini Kenya, Rigathi Gachagua.

Aliyekuwa Naibu Rais Nchini Kenya, Rigathi Gachagua amedai kuwa hayuko salama na kubainisha kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye chakula mara mbili.

Akizungumza na Televisheni ya Citizen akiwa anatoka katika Hospitali ya Karen alipokuwa anatibiwa, Gachagua amedai kuwa “Ruto hakuwa na nia ya kufanya kazi nami”, alitaka tu kunitumia kupata watu kushinda uchaguzi”,

“Kwa mara ya kwanza, niseme ilikuwa mnamo Agosti 30, huko Kisumu, walinzi wa siri waliingia chumbani kwangu Kisumu kwa nguvu na mmoja wao akajaribu kunitilia sumu kwenye chakula changu, lakini tuligundua na tukaweza kuepuka mpango huo.” Gachagua amesema.

“Nilitakiwa kuuawa kwa kuwekewa sumu, na mnamo Septemba huko Nyeri, timu nyingine ilikuja na kujaribu kunitilia sumu kwenye chakula ambacho kilichokusudiwa kuwa changu na Baraza la Wazee wa Kikuyu.”

Rigathi Gachagua ameendelea kumshutumu Rais William Ruto na kudai kuwa amesaliti makubaliano waliokuwa nayo kabla ya kuingia madarakani mwaka 2022.

“Ruto atawajibika iwapo lolote litanitokea” amesema Gachagua huku akiongeza kuwa alilazimika kuwatimua baadhi ya maafisa wa ujasusi katika ofisi yake kwa sababu hakujihisi salama.

Leave a Comment