×

Mwenezi Amos Makala Aibua Jambo Zito Kuhusu Tundu Lissu “Kiongozi Mkubwa Hajajiandikisha” – Video

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala amewashukia baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao mara kadhaa wamekuwa mstari wa mbele kujitokeza kukosoa muenendo wa uchaguzi huku, huku wenyewe wakiwa hawako tayari kuonyesha mfano katika ushiriki wa zoezi hilo

Amesema inashangaza kuona baadhi ya viongozi waandamizi wa vyama vya siasa vya upinzani wakishindwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa lililofungwa hivi karibuni, jambo ambalo moja kwa moja linawaondolea sifa ya kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi huo

Makala ambaye pia ni Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam amezungumza hayo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, taarifa aliyoipokea kutoka kwa viongozi wa CCM wa mkoa huo leo, Jumanne Oktoba 22.2024 ambapo katika kukoleza ajenda huyo amemtolea mfano Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara Tundu Lissu akidai kuwa ni miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao watakosa sifa ya kupiga kura kwa kuwa hajajiandikisha kwenye daftari hilo

Amesema ni jambo ambalo linashangaza kuona kiongozi wa kitaifa wa chama cha siasa ambaye kiuhalisia anapaswa kuwa mfano kwa wengine anashindwa kujiandikisha, huku upande wa pili kiongozi huyohuyo anajitokeza kukosoa michakato ya uchaguzi huo ambao yeye hakutaka kuwa sehemu ya washiriki.

Leave a Comment