
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani leo hii majira ya saa 1:00 usiku dhidi ya klabu ya JKT Tanzania katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
Yanga wamecheza michezo mitano ya Ligi Kuu hadi sasa na kushinda michezo yote ikiwemo ushindi wa goli 1-0 katika mchezo wa uliopita dhidi ya wapinzani wao Simba SC na kujikusanyia alama 15 wakiwa nafasi ya 3 katika msimamo.
JKT walio katika nafasi ya saba, wakiwa na alama 10 katika michezo saba, wataingia na kumbu kumbu nzuri baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Tabora United katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu ya NBC.
Katika michezo mitano ya mwisho iliyozikutanisha timu hizi, JKT imefanikiwa kupata sare mara mbili tu huku ikipoteza michezo mitatu ikiwemo kichapo kilali cha mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Agosti 29, 2023.