×

Padri kesi ya Asimwe Adaiwa Kuwa na Ugonjwa wa Akili

Washitakiwa  tisa (9)  wanaotuhumiwa kuhusuka na mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Marehemu Noela Asimwe Novat aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu mkazi wa  kata ya kamachumu ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera  wamefikishwa mbele ya jaji wa mahakamani kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusomewa shitaka linalowakabili na maelezo ya awali ya kesi hiyo kabla haijaanza kusikilizwa.

Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba Emanuel Ngingwana aliyekubaliana na maombi yaliyowasilishwa na upande wa jopo la mawakili wa utetezi ya mtuhumiwa namba moja padri Elipidius Rwegoshora kutosomewa  mashitaka   yanayomkabili hadi atakapofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili.

Jopo la mawakili wanne wa upande wa utetezi likiongozwa wakili msomi Projestus Mulokozi awali liliiiomba mahakama isitishe zoezi hilo kwa kuwa mteja wao kwa sasa hana uwezo wa kuongea vizuri pamoja na kuelewa anachokifanya kwa maana hiyo hawezi kujitetea kwa usahihi  hivyo wakaomba kupokelewa kwa  maombi ya upande wa utetezi yaliyotolewa.

Aidha mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Waziri Magumbo anayeshirikiana na mawakili wengine wa Serikali ambao ni pamoja na Erick Mabagala na Matilda Assey hawakuweka pingamizi la aina yoyote walikubaliana na uamzi uliotolewa na mahakama wa kusikitisha zoezi.

Jaji Ngigwana aliamua  mtuhumiwa apelekwe Isanga akapimwe akili hivyo,alieeleza kuwa watuhumiwa wote watasomewa mashtaka ya kesi inayowakabili kwa pamoja baada ya kupatikana matokeo ya uchunguzi wa ugonjwa wa akili wa mtuhumiwa namba moja padre Elipidius Rwegoshora ambapo kesi hiyo itatajwa tena Desema 11,mwaka huu.

Watuhumiwa wengine ni Novat  Venant (24) ambaye ni Baba mzazi wa mtoto  Asimwe,Ramadhan Selestine,Nurdin Masoud,Rwenyangira Burukad, Dastan Burchard,Faswiu Athman, Gozibat Arikad na Dezdery Everigist amabo wote wamerudishwa Lumande.

Leave a Comment