×

Simba, Azam Kushuka Dimbani Leo

Ligi Kuu ya Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo katika mikoa mbalimbali nchini ambapo vilabu vya Simba na Azam vinatarajiwa kushuka dimbani kusaka alama 3 katika mbio za ubingwa wa msimu huu.

Simba SC watakuwa wenyeji wa mchezo wao dhidi ya Namungo FC ya Lindi iliyo chini ya kocha Juma Mgunda ambae amewahi kukinoa kikosi cha wekundu wa msimbazi kwa nyakati tofauti tofauti katika mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba la KMC Complex kuanzia majira ya saa 10:15 alasiri.

Katika mchezo wa baadae, Azam FC watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex Chamazi kuwakaribisha KenGold ya Mbeya waliopanda daraja msimu huu, mchezo unaotarajiwa kuchezwa kuanzia majira ya saa 1:00 usiku.

Katika mchezo mwingine wa mapema leo hii, vinara katika msimamo wa Ligi Kuu, Klabu ya Singida Black Stars ambao mpaka sasa bado hawajapoteza mchezo wowote wakicheza michezo 7, na kushinda michezo 6 na kutoa sare mara moja watakuwa wenyeji dhidi ya Klabu ya Fountain Gate FC katika mchezo unaotarajiwa kupigwa katika dimba la CCM Liti mkoani Singida kuanzia majira ya saa 8:00 mchana.

Leave a Comment