×

Rais Samia Ashiriki mjadala kuhusu Kilimo barani Afrika, Iowa nchini Marekani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Corporation Bi. Alice Albright ambapo mazungumzo hayo yalijikita katika kukuza na kuimarisha mahusiano baina ya pande mbili hizo, tarehe 30 Oktoba 2024, Des Moines, Iowa nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.

Viongozi mbalimbali wakifuatilia mjadala kuhusu Kilimo Barani Afrika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation tarehe 30 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani Oktoba 30, 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.

MWITA (17) AKAMATWA AKIDAIWA KUMUUA RAFIKI YAKE MIAKA 18 KISA MAPENZI – KAMANDA AELEZA…

Leave a Comment