Mwanadada mrembo aliyejipatia umaarufu kupitia kazi yake ya ukondakta kwenye mabasi ya mikoani, Nice Moshi @naycemoshi, amesema kuwa hapendezwi kabisa na kitendo cha mtu kudharau kazi yake na kwamba alishawahi kumshtaki mtu na kumlaza kituo cha polisi kwa siku tatu kutokana na kumdhalilisha kwa maneno.