Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMIwSEMI na Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar na Sekretariet ya Mkoa wa Morogoro wakijadiliana jambo na wanakikundi cha UWASAMO jana. Morogoro, 6 Novemba 2024: Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar wamekitembelea Kikundi cha Ufugaji wa samaki kiitwacho UWASAMO kilichopo Mtaa wa Konga Kata ya Mzinga.
Lengo la safari hiyo lilikuwa ni kuona mafanikio ya ufugaji wa samaki kwa wanakikundi hao baada ya kupatiwa mafunzo ya Ufugaji samaki, biashara na utunzaji wa kumbukumbu kutoka Kituo cha Kingolwira.
Ziara hiyo imefanyika jana Novemba 6 mwaka huu kwenye kituo hicho kinachojishughulisha na utoaji mafunzo ya ufugaji samaki, pamoja na uuzaji wa vifaranga vya samaki.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi ndugu Asungushe Patrick Msugupakulya amesema, wao kama Wanakikundi wanaishukuru serikali kwa kuwaletea mradi wa IFAD, ambao umewasaidia katika kuunda ushirika wao ambao mpaka sasa wanaendelea kupata msaada wa elimu ya ufugaji wa samaki kwa wakati.
Pamoja na hayo Wanakikundi cha UWASAMO, wamefurahishwa na ziara ya viongozi hao, ambapo wanaamini kwa kutembelewa huko watapata misaada zaidi ya kuendeleza mtaji wao wa ufugaji wa samaki na kuwapatia maendeleo yenye tija kwa familia na Tanzania kwa ujumla wake. Alimaliza kusema.