
MWLIKI wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrance Mafuru aliyefariki Novemba 9, 2024 dunia, akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Apollo nchini India unaagwa leo Novemba 14, 2024 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anashiriki kuaga mwili wa Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango.
Mafuru aliyekuwa mtaalamu wa fedha na uchumi maarufu hapa nchini, amehudumu katika taasisi kubwa tofauti kwa miongo miwili. Amewahi kuwa Msajili wa Hazina na Ofisa mtendaji mkuu wa Benki ya NBC Tanzania.
Pia amewahi kuwa Naibu Katibu wa Wizara ya Fedha, Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki nchini (TBA) na mwanzilishi wa mwenza wa kampuni ya ushauri wa masuala ya fedha ya Bankable.




