×

Watoto wa Sinza Maalum Wakumbukwa kwa Misaada Mbalimbali

Dar es Salaam, 16 Novemba 2024: Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo Tanzania katika kuelekea kufunga mwaka, wametoa msaada wa vitu mbalimbali  kwenye Kituo cha Sinza Maalum kilichopo Jijini Dar, ambacho kina watoto zaidi ya 93.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Tigo mkoa wa Dar es Salaam, Aiden Komba amesema Tigo Tanzania inatambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalum na kuona ulazima wa kurejesha kwa jamii hiyo sehemu ya faida wanayoipata.
Msaada uliotolewa kituoni hapo ni pamoja na cherehani kadhaa, magodoro, chupa, ‘mahotipoti’ kwaajili ya kuhudumia jamii hiyo yenye uhitaji maalum.
Sanjali na hayo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Catherine Msese ametoa shukrani zake kwa Kampuni ya Tigo Tanzania kwa msaada huo waliowapatia kwaajili ya shule hiyo.
“Kwa kweli msaada huu utawasaidia sana watoto hawa kujimudu katika kufanya kazi zao za kila siku kwani sasa tumepata vifaa vya usafi ambavyo vitawasaidia katika kufanya usafi hapa shuleni na cherehani ambazo zitawasaidia katika mafunzo ya ufundi,” alisema.
Sehemu ya msaada huo.
Kampuni ya Tigo Tanzania katika kuendeleza kurudisha kwa jamii sehemu ya faida inayoipata, itaendelea kutoa misaada hiyo kwa kanda zote tisa nchini ambapo wameanzia kituo hicho kwa kanda ya Dar es Salaam.

Leave a Comment