×

Gamondi Afungiwa Michezo Mitatu na Kumtoza Faini ya Tsh Milioni 2

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB imetangaza kumfungia aliyekuwa kocha wa Young Africans Sc, Miguel Angel Gamondi michezo mitatu na kumtoza faini ya Tsh Milioni 2 kwa kosa la kumpiga na kumuangusha Kocha Msaidizi wa klabu ya Singida Black Stars kwenye mchezo baina ya timu hizo uliochezwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Adhabu hiyo inamkuta Gamondi akiwa kwenye mlango wa kutokea baada ya kufutwa kazi kama kocha mkuu wa Wananchi.

Leave a Comment