
Kufuatia tukio baya la kuanguka kwa jengo la ghorofa Mtaa wa Kongo na Mchikichi jijini Dar jana na kuua na kujeruhi watu kadhaa zoezi la uokoaji bado linaendelea mpaka muda huu.
Mwanahabari wetu akiwa eneo hilo muda mfupi uliopita alishuhudia vikosi mbalimbali vya uokoaji kama vile Chama cha Msalaba Mwekundu ‘Redcross’, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Askari wa Uhamiaji, Magereza, Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa ‘JKT’, JWTZ pamoja na vijana wa Scout wote kwa pamoja wakiendelea kushirikiana kujaribu kuwaokoa baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa chini ya kifusi cha jengo hilo.
Wakati vikosi hivyo vikiendelea na uokoaji magari ya uokoaji na Ambulance kutoka hospitali mbalimbali nazo zimeonekana kwa wingi eneo la tukio tayari kwa ajili ya kuwahisha majeruhi na miili ya waliofariki hospitalini. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL



