Mwili wa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Boniface Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kwa jina la King Kikii unaagwa leo Novemba 18, 2024 katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
King Kikii alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Miongoni mwa nyimbo za King Kikii zilizotamba sana ni ‘Kitambaa Cheupe’.