×

Waokoaji Janga la Kariakoo Waendelea Kupigwa Tafu na Wadau

Maneja Mkuu wa Mahesabu OYA  Mr. Alfa Chiwanga  (kushoto) akiwa na  Meneja Rasilimali Watu wa OYA, Regina Maduka wakikabidhi msaada wa mahitaji muhimu kwenye zoezi la uokoaji linaloendelea Kariakoo jijini Dar.

Dar es Salaam, 23 Novemba 2024: Uongozi wa OYA na wafanyakazi wake wameungana na Watanzania wengine kutoa mchango wao kwenye kuunga mkono juhudi zinazoendelea kutolewa za uokoaji kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa eneo la Kariakoo jijini Dar, Jumamosi iliyopita na kusababisha maafa makubwa ikiwemo vifo kadhaa na majeruhi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Regina Maduka alisema;

“Tunaungana na jamii nzima ya Watanzania katika kudumisha utamaduni wetu wa kushirikiana kwenye changamoto kama hizi kwa kutoa pole sana kwa waliopoteza wapendwa wao kwenye janga hili.” Alisema Regina.

Aliendelea kusema; “Siku ya leo tumesimama pamoja na jamii nzima ya Watanzania haswa walioathirika na janga hili tukidumisha utamaduni wetu wa mshikamano na upendo kwenye kukabiliana na changamoto kama hizi.

Tunatoa pole sana kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao na tutaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha msaada kama huu unafika pale unapohitajika. Watanzania sisi sote ni ndugu na kwa pamoja tunaweza kutengeneza Tanzania iliyo bora zaidi”. Alimaliza kusema Regina.

Leave a Comment