Klabu ya soka ya Yanga imekubali kichapo cha mabao 0-2 kutoka Kwa Al Hilal ya nchini Sudan, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Hiki ni kichapo cha tatu mfululizo Kwa miamba hiyo ya Twiga na Jagwani, baada ya kupoteza michezo miwili ya ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam FC na Tabora united.
Huu unakuwa ni mwanzo mbovu kwa kocha mpya wa Klabu hiyo Sead Ramovic aliyechukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo kutoka kwa muargentina Miguel Gamondi aliyetimuliwa baada ya mwenendo mbovu wa klabu hiyo.
Matokeo hayo yanaifanya Al Hilal kukaa kileleni katika msimamo wa kundi A, baada ya Tp Mazembe na Mc Alger kutoka sare ya bila kufungana kule nchini DR Congo.