Spika wa Bunge la Guinea Ahukumiwa Miaka 4 jela na faini

Baada ya kesi ya zaidi ya miaka Miwili, Spika wa zamani wa Bunge la Guinea, Amadou Damaro Camara, amehukumiwa na Mahakama ya makosa ya Uchumi na Fedha kwa vitendo vya ubadhirifu wa Mali, Fedha za umma na rushwa.
Baada ya kujadiliwa, Mahakama hiyo inayoongozwa na Jaji Yacouba Conté, ilitoa hukumu ya miaka 4 jela na faini ya Faranga Milioni 10 za Guinea dhidi yake.
Zaidi ya hayo, mahakama iliamuru kukamatwa kwa mali zake.
Washitakiwa wenzake katika kesi hii, Michel Kamano, ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi kwa sababu za kimatibabu, alihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa mambo sawa na hayo, ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa fedha za umma, ufisadi na utajiri haramu.
Mbali na kifungo chake jela, atalazimika kulipa faini ya faranga bilioni 4 za Guinea.

