
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limethibitisha kuwa Treni zake tatu ikiwemo Treni yake ya ‘Mchobgoko’ zilisimama kufanya kazi kwa muda leo asubuhi Desemba 04, 2024 kutokana na kuathiriwa na hitilafu ya umeme kwenye Gridi ya Taifa lakini kwa sasa umeme umerejea na Treni zinaendelea na safari zake.
