
Dar es Salaam, Tanzania, 05 Disemba 2024 – Najali Care, jukwaa la kibunifu la utalii wa matibabu la Afrika Kusini, na American Clinic, mtoa huduma wa afya maarufu Tanzania, wametangaza ushirikiano wa kimkakati ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na uvumbuzi kwenye sekta ya afya barani Afrika.
Ushirikiano huu unalenga kusaidia wagonjwa kwa kuunganishwa na madaktari bingwa na wataalamu wa matibabu ya hali ya juu, kuwapatia wagongwa huduma za kidijitali na kuboresha utoaji huduma za afya baina ya nchi za Afrika, ikianza na Tanzania na Afrika ya Kusini.
Kwa kutumia utaalamu wa Najali Care katika usimamizi wa kuunganisha wagonjwa na madaktari bingwa na sifa ya American Clinic katika sekta ya afya, ushirikiano huu unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa na kujenga mifumo ya afya ya kidijitali kwa ujumla.

Dk. Nandipha Ndhlovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Najali Care, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu akisema, “Ushirikiano huu ni hatua muhimu kuelekea kuboresha huduma za afya pale mgonjwa anapohitaji msaada nje ya mipaka ya nchi yake.
Kwa kuunganisha utaalamu wetu wa kiutawala kwenye sekta ya afya na viwango vya huduma bora vya American Clinic, tunahakikisha kuwa wagonjwa wanapata msaada wa kina—kuanzia ushauri wa huduma inayostahili kutolewa kabla ya matibabu kuanza, mipango ya safari hadi huduma za ufuatiliaji wakati na baada ya matibabu. Zaidi ya hayo, ushirikiano huu unaimarisha mifumo y afya baina ya nchi hizi mbili, kupitia kubadilishana maarifa na kujengeana uwezo, na hivyo kuimarisha nafasi ya Afrika katika ubunifu wa huduma za afya duniani.”
Ushirikiano huu unawapa wagonjwa huduma mbalimbali, ikiwemo ushauri wa awali ya matibabu, usafiri ulioratibiwa na malazi, na upatikanaji wa matibabu maalum nchini Afrika Kusini. Wagonjwa pia watanufaika na huduma za ufuatiliaji baada ya matibabu kabla ya kurejea nchini, na pale wanaporudi nchini kuhakikisha muendelezo wa huduma.
Violet Luwanja, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa hospitali ya American Clinic, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kusaidia vipaumbele vya kitaifa vya afya kwa kusema;
“Ushirikiano huu unakamilisha jitihada za serikali ya Tanzania za kuboresha utoaji wa huduma za afya na kupanua upatikanaji wa huduma bora.
Pamoja na Najali Care, hatujajikita tukwenye kuwezesha upatikanaji wa matibabu ya hali ya juu bali pia tunawekeza katika ukuaji wa muda mrefu wa mfumo wetu wa afya kupitia mafunzo ya wataalam, kubadilishana maarifa, na uvumbuzi wa kidijitali. Dira yetu ya pamoja ni kusaidia huduma za afya endelevu na jumuishi ambazo zinatoa thamani kwa wagonjwa na watoa huduma kwa ujumla.”
Ushirikiano huu pia unaleta suluhisho la kidijitali lililobuniwa na kampuni ya teknolojia ya afya inayojulikana kama Afya Rekod, itakayowezesha wagonjwa kuhifadhi na kupata taarifa zao za afya kirahisi, pamoja na kupata huduma za afya na ushauri kutoka kwa wataalamu bingwa kupitia kwenye platfom muda wowote na mahali popote.
Maendeleo haya yanahakikisha kuwa huduma za afya zinapatikana kwa wagonjwa kote barani, huku pia yakitoa fursa za ukuaji wa kitaaluma na ushirikiano kwa wataalam wa afya wa ndani nanje ya nchi.
Afya ya kinga ni msingi mwingine wa ushirikiano huu, kupitia kampeni za afya za kijamii na mipango ya kuwezesha wagonjwa kugundua mapema magonjwa ya muda mrefu, kama saratani, na magonjwa ya moyo. Warsha za elimu na uchunguzi wa afya zitakazotolewa zitasaidia jamiikujikita kwenye kudhibiti afya zao.
Ushirikiano pia utaleta madaktari bingwa wageni kwenye nyanja kama vile oncology, cardiology, na gynecology, aesthetics, neurologynk. kutembelea Tanzania, na kuwezesha mafunzo ya kitaalam na programu za ushauri ili kuleta maendeleo ya ujuzi wa ndani na kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania.
Soko la utalii wa matibabu linakadiriwa kuwa dola bilioni 180 duniani kufikiamwaka 2026, Najali Care na American Clinic Tanzania wanaonyesha njia ya kuhakikisha Afrika haikai nyuma kwenye kujikita kwenye soko hili kwa kuweka mifumo ya kujijenga kwenye kujihudumia na kuhudumia dunia.
Dk. Ndhlovu alihitimisha kwa kusema “Tunajikita kujenga mfumo wa huduma za afya unaoonyesha uwezo wa Afrika kama mtoaji na mvumbuzi wa suluhisho za matibabu za kiwango cha dunia. Ushirikiano huu hauhusu tu kuziba mapengo—unajumuisha kuunda mifumo endelevu ambayo itajenga matumaini na kuleta suluhisho za kiwango cha juu kwa jamii kote barani.”
Kuhusu Najali Care:
Najali Care ni jukwaa la utalii wa matibabu na usimamizi wa huduma za afya la Afrika Kusini lililojikita kusaidia wagonjwa kuunganishwa na madaktari bingwa Africa ya Kusini, pamoja na kuunda kujengea uwezo watoa hudiuma za afya kama vituo vya afya na hospitali kote barani Afrika. Kwa kuwaunganisha wagonjwa na wataalam bingwa na vituo vya huduma, Najali Care inachangia kutoa matokeo bora ya afya kwa jamii na sekta.
Kuhusu American Clinic:
American Clinic ni mtoa huduma wa afya nchini Tanzania, anayetoa huduma mbalimbali za matibabu za hali ya juu, ikiwa ni pamoja na uchunguzi, upasuaji, na usimamizi wa magonjwa ya muda mrefu. American Clinic ina dhamira ya kutoa huduma bora na kujenga uvumbuzi was eka ya afya, ikiunga mkono Serikali ya Tanzania kwenye kuhakikisha inakuza afya na ustawi wa jamii zote Tanzania