Tamasha kubwa la Kula Bata lililopewa jina la Bata la Disemba si mchezo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia tamasha hilo la siku tatu linaloendelea mpaka sasa kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar.
Katika tamasha hilo lililosheheni vyakula na vinywaji vya kila aina limenogeshwa na burudani kutoka kwa bendi na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya.
Miongoni mwa waliotoa burudani mpaka sasa ni Kundi la Weusi lenye maskani yake Arusha na Dar, mwanadada mkali kutoka South Afrika Char4Prezzy, Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiwa na mastaa wake wote kama vile, Chalz Baba, Luiza Mbutu, Dogo Rama na wengineo.
Wakati burudani hizo zikiendelea kuku choma wa kienyeji ‘vyuku’, Mbuzi na makulaji mengine nayo yalikuwa yakiwasubiri walaji kila kona ya kiwanja hicho kilichokusanya mastaa na watoto wa mjini kibao. Msanii aliyezolea umaarufu kupitia mitandao ya kijamii Doto Magari naye alionekana kuvinjali kiwanja hicho kwa ajili ya kula bata.
Tamasha hilo leo Jumapili ndiyo kumekucha kabisa Bata la kufa mtu linaendelea kwenye kiwanja hicho maarufu kilichokusanya raha zote za jiji la Dar.
HABARI NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL PUBLISHERS





Watu wakila bata