
Mchekeshaji wa Mtandaoni maarufu, Frank Patrick ‘Molingo’ (17) mkazi wa wilaya ya Chato Mkoani Geita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 10,2024 akiwa nyumbani kwao ambako alikuwa akiuguzwa na mama yake mzazi.
Rafiki yake ambaye alikuwa akiishi nae na kumrekodi vichekesho vyake Mudi Msomali amesema kuwa Molingo alikuwa anaugua mara kwa mara na chanzo cha ugonjwa bado hakijajulikana huku akisema muda mwingine alikuwa anavimba mwili na kuishiwa damu Mwilini.